Vikosi vya ulinzi vya Uganda siku ya Jumatatu, vilishambuliwa na wapiganaji wasiojulika, katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Vikosi hivyo ambavyo ni sehemu ya vikosi vya usalama vya Jumuiya ya Afrika Mashariki, vinavyodumisha amani mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC, vilishambuliwa katika eneo la Rukoro.
Hata hivyo, kupitia kwa taarifa, Kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki EACRF, kilisema wanajeshi hao wa Uganda walikabiliana na wapiganaji hao na kuwashinda nguvu, kabla ya kuendelea na safari yao salama.
Kulingana na taarifa hiyo, uchunguzi umeanzishwa kuwatambua wapiganaji hao na lengo la shambulizi hilo.
EACRF ilisema itaendelea kutekeleza jukumu lake la kuwalinda raia na halitasita kutumia nguvu iwapo maisha ya wanajeshi wake yatakuwa hatarini.
Kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki, kilipelekwa kukabiliana na waasi wa M23, Mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.