Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi nchini Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ametangaza kwamba hatogombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2026.
Kupitia mtandao wa X, Muhoonzi alisema Mweneyzi Mungu amemzungumzia na kumweleza ahudumie jeshi la nchi hiyo, na kwamba atamuunga mkono Rais Yoweri Museveni kuwania wadhifa huo.
“Ningependa kutangaza kwamba sitakuwa kwenye uwaniaji uongozi wa uchaguzi wa 2026. Mwenyezi Mungu ameniambia nihudumie jeshi la nchi hii. Kwa hivyo namuunga mkono Rais Yoweri Museveni kikamilifu,” alisema Jenerali Muhoozi.
Hapo awali, Jenerali Muhoozi alikuwa ameashiria kuwa atawania Urais wa taifa hilo, kumridhi babake Rais Museveni katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2026.
“Mumekuwa mkisubiri niseme……haya basi nitawania urasi katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2026,” alisema Muhoozi katika ukurasa wa X hapo awali, kabla ya kubadili msimamo huo.
Muhoozi aliteuliwa kuwa Mkuu wa Vikosi vya ulinzi nchini Uganda mwaka 2024, hatua iliyoibua hisia mseto nchini humo.