Jenerali Charles Muriu Kahariri ateuliwa mkuu mpya wa majeshi ya Kenya

Marion Bosire
2 Min Read

Rais wa Jamhuri ya Kenya William Samoei Ruto amempandisha cheo Charles Muriu Kahariri hadi kiwango cha Jenerali na kumteua kuwa mkuu mpya wa majeshi ya Kenya KDF.

Haya ni kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye akaunti rasmi ya KDF kwenye mtandao wa X ambayo ilikunuu taarifa rasmi kwa vyombo vya habari kutoka kwa wizara ya ulinzi.

Jenerali Kahariri akiapishwa kuwa naibu mkuu wa majeshi Machi 9, 2024

Wengine walioathiriwa na mabadiliko katika jeshi hivi leo ni pamoja na Meja jenerali John Mugaravai Omenda ambaye amepandishwa cheo na kuwa Lieutenant General na kuteuliwa kuwa naibu mkuu wa majeshi ya Kenya.

Kabla ya uteuzi wa leo, Jenerali Omenda alikuwa akihudumu kama kamanda wa jeshi la wanahewa.

Meja Jenerali Fatuma Gaiti Ahmed amehamishiwa jeshi la wanahewa na kufanywa kamanda huku Meja Jenerali Paul Owuor Otieno akihamishiwa jeshi la wanamaji na kuteuliwa kamanda.

Chuo kikuu cha ulinzi nchini kimepata naibu chansela mpya kwa jina meja jenerali Thomas Njoroge Ng’ang’a ambaye atahusika na masuala ya usimamizi na fedha.

Brigedia Peter Nyamu Githinji amepandishwa cheo kuwa meja jenerali na kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa masuala ya angani katika taasisi ya mafunzo ya ulinzi nchini.

Jattani Kampare Gula naye amepandishwa cheo kutoka kiwango cha Brigedia hadi meja jenerali, sawa na wenzake George Okumu na Samuel Kosgei Kipkorir.

Gula ameteuliwa kusimamia kiwanda cha nyama cha serikali Kenya Meat Commision, Okumu ameteuliwa kusimamia kiwanda cha Kenya Orchance Factories Corporation and Food Processing factoru huku Kipkorir akifanywa kuwa naibu kamanda wa jeshi la wanahewa.

Website |  + posts
Share This Article