Jamii ya Wapemba yapewa uraia Kenya

Dismas Otuke
1 Min Read

Wapemba zaidi ya laki moja wanaoishi nchini wamepewa uraia kuwa mojawapo ya makabila ya Kenya.

Wapemba wamekuwa wakiishi nchini kwa miongo kadhaa ila hawajapewa kibali na kutabuliwa kuwa Wakenya kisheria huku idadi ndogo ya watu wapatao 7,000 wakisajiliwa.

Wapemba sasa wako huru kuwa na kitambulisho cha kitaifa na stakabadhi nyinginezo.

Idadi kubwa ya Wapemba inapatikana maeneo ya Kwale, Kilifi na Mombasa huku wachache wakizagaa Nakuru, Homabay na Kisumu.

Jamii hii ni maarufu kwa uvuvi, upigaji mbizi na kuendesha mashua .

Asili ya Wapemba ni kisiwani Zanzibar nchini Tanzania na waliingia nchini Kenya nyakati za Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *