James Mwangi ateuliwa chansela wa Open University

Dismas Otuke
1 Min Read

Afisa Mkuu Mtendaji wa benki ya Equity Group Dkt. James Mwangi ameteuliwa kuwa chansela wa chuo cha kwanza cha kutoa mafunzo kupitia mtandaoni maarufu kama Open University.

Makao makuu ya chuo hicho yatakuwa katika kiwanda cha Konza, kaunti ya Machakos.

Akitangaza uteuzi wake leo Alhamisi, Rais William Ruto amesema ana imani na utendakazi wa Dkt. Mwangi kupeleka chuo hicho hadi katika upeo wa juu.

Mwanataalum Ezra Martin aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa baraza la chuo hicho.

Ruto alisema haya alipotoa hati ya chuo hicho kuwa chuo kikuu cha umma.

Website |  + posts
Share This Article