Jamaa mmoja ambaye ni fundi wa magari katika mji wa Narok, alifariki papo hapo baada gurudumu alilokuwa akitengeneza kulipuka na kumrusha hewani na kisha akaanguka chini kwa kishindo kikubwa na kufariki.
Shinikizo la hewa ambayo ilikuwa ndani ya gurudumu hilo ndilo lilisababisha hali hiyo.
Kichwa chake ndicho kilitangulia chini alipoanguka.
Kisa hicho ambacho sio cha kawaida kiliwashangaza wanabiashara mjini Narok kwani kichwa cha mwathiriwa kilipasuka vipande vipande.
Kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Narok ya kati John Momanyi alithibitisha kisa hicho huku akihimiza mafundi wawe wakivaa mavazi ya kujikinga kama kofia ili kuzuia visa kama hivyo.