Mahakama ya Nyahururu imemtoza mwanamume wa umri wa makamo faini ya shilingi milioni 50 au kifungo cha miaka 30 kwa kuhifadhi bangi ya shilingi milioni 41 katika kijiji cha Kigumo – Lusogwa – Nyahururu kaunti ya Laikipia.
wakati wa kesi hiyo, mashahidi watano walitoa ushahidi dhidi ya mshatakiwa na ambao mawakili wake walishindwa kukanusha.
kufuatia hatua hiyo, hakimu mkaazi wa Nyandarua Fredrick Larabi alitoa hukumu hiyo kwa kusema kuwa, ” kufuatia ushahidi, nimepata kuwa mwendesha mashtaka amethibitisha mashtaka dhidi ya mshatakiwa. Ushahidi uliotolewa umeshawishi kutolewa kwa hukumu ya usafirishaji wa dawa za kulevya na mshatakiwa. Mshatakiwa amepatikana na hatia kama vile alivyohukumiwa na atafungwa chini ya kifungu 215 CPC ” Alisema Larabi.
hata hivyo, alipewa siku 14 kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
mahakama pia iliamuru mifuko 63 ya bangi iliyowasilishwa kama ushahidi kuharibiwa chini ya usimamizi wa kamishina wa kaunti hiyo, kamanda wa polisi wa eneo hilo, mkurugenzi wa ucghunguzi wa uhalifu – DCI, mkuu wa kituo cha polisi cha Nyahururu – OCS na afisa wa afya.
Hakimu vile vile, aliamuru mabati na shehena iliyotumiwa kuhifadhi bangi hiyo kuwasilishwa mahakamani kwa matumizi mengine kwa kuwa hakuna aliyedai kuwa yake.