Jamaa afungwa miaka 30 jela kwa kuua Padri

Padri Michael aliuawa Oktoba 8, 2019 wakati huo akihudumu katika Parokia ya Thatha iliyoko Masinga, kaunti ya Machakos.

Marion Bosire
1 Min Read

Kavivya Mwangangi mshtakiwa wa pili wa mauaji ya padri wa kanisa katoliki Michael Kyengo Maingi amehukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani.

Padri Michael aliuawa Oktoba 8, 2019 wakati huo akihudumu katika Parokia ya Thatha iliyoko Masinga, kaunti ya Machakos.

Hukumu ya Kavivya Mwangangi ilitolewa mapema jana katika mahakama kuu ya Embu na jaji L. Njuguna, kufuatia kukamilika kwa vikao vya kusikiliza kesi hiyo iliyoanza mwaka 2019.

Mwezi Julai mwaka 2021, mahakama ilimhukumu mshtakiwa wa kwanza wa kesi hiyo Michael Muthini Mutunga, kifungo sawia cha miaka 30 gerezani baada yake kukiri mashtaka.

Katika kujitetea Muthini ambaye alikuwa mwanafunzi wa taasisi ya elimu ya juu, alisema kwamba akimuua Padri Maingi kwa sababu ya kumdhulumu kingono, madai ambayo jaji Njuguna alipuuzilia mbali.

Jaji alisema madai hayo hayangedhibitishwa na kwamba iwapo angedhulumiwa kingono, Muthini angetumia mbinu za kisheria kupata haki.

Anadaiwa kutoa pesa kwenye akaunti za benki za marehemu Padri na hata kutumia gari lake kwa muda baada ya kumuua.

Muthini alikamatwa na maafisa wa polisi siku chache baada ya kutekeleza unyama huo lakini akaachiliwa kwa dhamana.

Julai 10, 2021, maafisa wa polisi walimkamata tena kwa kutekeleza kitendo hicho cha kinyama.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *