Jamaa afungwa maisha baada ya kupinga kifungo cha miaka 30

Marion Bosire
1 Min Read

Charles Musau Mang’eli amejiongezea dhiki baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani kufuatia hatua yake ya kukata rufaa kwa kifungo cha awali cha miaka 30 akisema ni adhabu kali kwake.

Mang’eli anasemekana kumbaka mtoto msichana wa miaka 6 Oktoba 4, 2017 katika eneo la Athi River mashtaka ambayo alikana mbele ya mahakama.

Siku ambayo kisa hicho kilitokea, mshtakiwa alikuwa amehudhuria mkutano wa chama ambao ulikamilika saa tisa alasiri kabla ya kutekeleza kitendo hicho.

Akijitetea mahakamani, mshtakiwa alikana kutekeleza kitendo hicho kilichotekelezwa saa 10 alasiri akisema alikuwa kwenye mkutano wa chama hadi saa 11 jioni.

Mwenyekiti wa chama chao alimtetea mahakamani ambapo alitoa ithibati ya stakabadhi za mkutano kwamba ulikwisha saa 11 jioni lakini mahakama ikampata na hatia na kumhukumu kifungo cha miaka 30 gerezani, Januari 29, 2023.

Badala ya kifungo cha maisha gerezani, alihukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani.

Hapo ndipo aliamua kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo na sasa amerejeshewa kifungo cha awali cha maisha gerezani!

Website |  + posts
Share This Article