Jaji wa Mahakama Kuu Daniel Ogembo afariki

Martin Mwanje
1 Min Read

Idara ya Mahakama kwa mara nyingine imepata pigo kufuatia kifo cha Jaji Daniel Ogembo. 

Hadi kifo chake, Jaji Ogembo alisimamia Mahakama Kuu ya Siaya.

Ripoti za kifo chake zimetolewa na Gavana wa Siaya James Orengo.

“Naungana na idara yote ya mahakama kuomboleza kifo cha Jaji Daniel Ogembo Ogola ambaye alisimamia Mahakama Kuu ya Siaya,” alisema Gavana Orengo kupitia mtandao wa X.

“Jaji Ogembo alikuwa na uwezo wa kustaajabisha wa kusikiliza kwa kudhamiria, kuakisi kimyakimya na kisha kuuliza maswali, mara kwa mara kwa maneno machache ambayo yalileba ubayana mahakamani. Na roho yake ilale mahali pema peponi.”

Inasemekana kwamba Jaji Ogembo alipatikana akiwa amefariki nyumbani kwake.

Kifo cha Jaji Ogembo kinakuja wakati idara ya mahakama inaomboleza kifo cha Jaji David Majanja ambaye mazishi yake yamepangwa kufanyika leo Jumatano.

Siku chache zilizopita, idara ya mahakama ilikumbwa na msiba mwingine baada ya Hakimu Mkuu Monica Kivuti kupigwa risasi na kuuawa katika mahakama ya Makadara.

Website |  + posts
Share This Article