Jaji David Majanja kuzikwa leo Jumatano

Tom Mathinji
1 Min Read
Marehemu Jaji David Majanja.

Jaji wa Mahakama kuu David Majanja, atazikwa leo Jumatano kuambatana na wasia wake.

Katika wasia huo, Jaji Majanja alisema mwili wake uchomwe moto baada ya kufariki.

Hafla ya kuchoma mwili wake itaandaliwa faraghani katika makafani ya Kariokor, ambapo ni familia yake tu itahudhuria.

Majanja ambaye alikuwa kamishna katika tume ya kuwaajiri wahudumu wa idara ya mahakama JSC, alifariki wiki iliyopita alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali moja Jijini Nairobi.

Ibada ya kumkumbuka Jaji hiyo itaandaliwa siku ya Jumamosi katika eneo bunge la Shinyalu, kaunti ya Kakamega.

Jaji Majanja amekuwa akihudumu katika mahakama kuu tangu mwaka 2011 na kituo chake cha hivi punde zaidi ni mahakama za Milimani.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *