Jaji David Majanja afariki

Marion Bosire
1 Min Read

Jaji wa mahakama kuu David Majanja amefariki. Kifo chake kilijiri leo Jumatano Julai 10, 2024, baada ya upasuaji aliofanyiwa katika hospitali ya Nairobi.

Jaji Majanja amekuwa akihudumu katika mahakama kuu tangu mwaka 2011 na kituo chake cha hivi punde zaidi ni mahakama za Milimani.

Amekuwa akihudumu kwenye tume ya huduma za idara ya mahakama JSC ambapo aliteuliwa kuwakilisha chama cha majaji na mahimu mwaka 2019 kabla ya kuteuliwa tena mwisho wa mwezi Mei mwaka huu.

Majanja ambaye katika utendakazi wake kama mwanasheria alipendelea masuala ya kiraia, kibiashara na yanayohusu umma alisomea katika shule ya Hill School huko Eldoret na shule ya upili ya kitaifa Alliance.

Shahada yake ya kwanza ya sheria aliipata katika chuo kikuu cha Nairobi huku ile ya uzamili akiipata kutoka chuo kikuu cha Pretoria nchini Afrika Kusini.

Alisomea pia diploma katika taasisi ya sheria nchini yaani Kenya School of Law na akafuzu kuwa wakili mwaka 1998.

Aliwahi kufanya kazi kwenye kampuni ya uwakili ya Mohammed and Muigai Advocates na ile ya Onyango and Ohaga Advocates na baadaye akaanzisha kampuni yake kwa jina Majanja Luseno and Company Advocates.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *