Jackie Maribe na Joseph Irungu kufahamu hatima yao tarehe sita Oktoba

Tom Mathinji
1 Min Read
Joseph Irungu na Jackie Maribe. Picha/Hisani

Justice Grace Nzioka wa mahakama kuu, ana muda wa miezi miwili na nusu kutoa hukumu kuhusu kesi ya mauaji ya mwanabiashara Monica Kimani, aliyeuawa kinyama mwaka 2018.

Hii ni baada ya kiongozi wa mashtaka na mawakili wa upande wa utetezi kujizatiti kuteta upande wao wakati wa mawasilisho ya mwisho, kabla ya mahakama kuanza kuandaa uamuzi utakaowasilishwa tarehe sita mwezi Oktoba mwaka 2023.

Katika mawasilisho yake ya mwisho, kiongozi wa mashtaka  Gichui Gikui, aliitaka mahakama kumpata aliyekuwa mtangazaji wa runinga Jackie Maribe na mpenzi wake Joseph Irungu na hatia ya mauaji ya mwanabiashara Monica Kimani.

Gichui alisema bunduki iliyotumika katika mauaji hayo, iliwasilishwa mahakamani huku ripoti ya uchunguzi wa DNA iliyoonyesha sampuli za damu zilizopatikana kutoka kwa Irungu, iliambatana na ile ya mwenda zake.

Hata hivyo, wakili wa Maribe Katwa Kigen, alimwambia jaji huyo kuwa upande wa mashtaka haukutoa ushahidi kumhusisha mteja wake na mauaji ya Monica.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *