Israel yaanzisha mashambulizi ya ardhini Syria

Tom Mathinji
1 Min Read
Daniel Hagari, msemaji wa jeshi la Israel.

Israel Jumapili imesema imeanzisha uvamizi wa ardhini Syria, kushikilia kile kilichoelezwa na Syria kujihusisha na mitandao ya Iran inayowasaidia wanamgambo katika eneo hilo.

Uvamizi wa Israel, nchini Syria, umekuwa wa kwanza katika kipindi cha miezi mitatu ya mgogoro wa mashariki ya kati. Syria haikujibu kwa haraka kuthibitisha madai ya oparesheni hiyo.

Jeshi la Israel haikusema sehemu ambapo uvamizi huo umefanyika ama muda, lakini imemtaja mtu iliye mshikilia kuwa ni Ali Soleiman al-Assi, na inaelezwa kuwa amekuwa akiishi katika mkoa wa kusini wa Syria, wa Saida.

Israel imesema alikuwa chini ya uchunguzi wa kijeshi kwa miezi kadhaa, na alijihusika katika juhudi za Iran, na kulenga maeneo ya Israel yenye mgogoro ya milima ya Golani karibu na mpaka wa Syria, jeshi limesema.

Picha za video za tukio hilo zilizotolewa zimeonyesha mtu huyo akishikiliwa ndani ya jengo moja.

TAGGED:
Share This Article