Israel: Mateka 31 waliozuiliwa gaza waliuawa

Tom Mathinji
1 Min Read
Daniel Hagari, msemaji wa jeshi la Israel.

Msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari, amesema kuwa mateka wasiopungua 31 walioshikiliwa huko Gaza waliuawa wakati wa vita vinavyoendelea katika Ukanda huo tangu Oktoba mwaka jana.

Hagari alieleza wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jumanne jioni kwamba, jeshi la Israel lilifahamisha familia za mateka 31 wa mauaji yao.

Israel inasema kuwa mateka 136 bado wanashikiliwa Gaza tangu Oktoba 7, na inatafuta kuwakomboa kupitia makubaliano na Hamas, au kupitia operesheni za kijeshi inazoendesha katika Ukanda huo.

Israel ilianzisha mashambulizi dhidi ya kundi la Hamas katika eneo la Gaza mwezi Oktoba mwaka 2023, baada ya wapiganaji wa Hamas kuishambulia Israel na kuwateka nyara raia kadhaa wa Israel.

Share This Article