Duru za kijeshi za Marekani zinaripoti kuwa meli ya mizigo inayomilikiwa na bilionea wa Israel imeshambuliwa na ndege isiyo na rubani na kusema, “Drone hiyo inashukiwa kuwa ya Iran.”
Afisa mmoja wa kijeshi aliyezungumza na shirika la habari la Associated Press kwa sharti la kutotajwa jina, alisema meli hiyo ililengwa ikiwa katika maji ya kimataifa na ndege isiyo na rubani ya Shahed-136 iliyokuwa imebeba bomu.
Kulingana na afisa huyo, ndege hiyo isiyo na rubani ililipuka na kusababisha uharibifu 2 wa meli hiyo bila ya kuwajeruhi wafanyakazi wake.
Kituo cha habari cha Al-Mayadeen kiliripoti kuwa meli ya mizigo ya Israel ilishambuliwa kaskazini mwa Bahari ya Hindi usiku wa kuamkia leo, saa chache kabla ya kuanza kwa usitishaji vita, tukio ambalo lilithibitishwa na vyombo vya habari vya Iran.