Iran yarusha makombora nchini Israel

Tom Mathinji
1 Min Read

Katika kile kinachoonekana kuwa hatua ya kulipiza kisasi mauaji ya kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh, na vile vile mauaji ya kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah, Iran imerusha makombora katika mji mkuu wa Israel, Tel Aviv.

Kulingana na Iran, mashambulizi hayo ya angani yalilenga kambi muhimu nchini Israel, ikisema kuwa haitasita kurusha makombora zaidi iwapo Israel itajibu mashambulizi hayo.

Hata hivyo jeshi la ulinzi la Israel IDF, limewataka raia wake kuwa makini na kuchukua tahadhari kwa kufuata maelezo ya kiusalama wanayopewa.

“king’ora kinapotoa sauti, enda eneo salama, hadi maelezo zaidi yatakapotolewa,” ilisema IDF

Israel imelaumiwa kwa kumuua kiongozi wa Hamas Haniyeh mwezi Julai mwaka huu, pamoja na kiongozi wa Hezbollah Nasrallah Ijumaa wiki jana.

Mashambulizi ya Israel katika maeneo ya Gaza na Lebanon, yamesababisha vifo vya watu wengi, huku takribani watu milioni moja wakihama makwao nchini Lebanon.

TAGGED:
Share This Article