Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula ametoa wito wa kufanya marekebisho katika sekta ya elimu, akitaja sekta hiyo kuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya taifa hili.
Spika huyo aliyasema hayo leo Jumatano afisini mwake katika majengo ya bunge baada ya kuwa mwenyeji wa ujumbe kutoka Chuo Kikuu cha Daystar.
Ujumbe huo uliongozwa na nNaibu Chansela wa chuo hicho Prof. Laban Ayiro.
Mkutano huo uliangazia maswala muhimu miongoni mwayo, utumizi mbaya wa fedha, haja ya kufanyia sera marekebisho na jukumu la vyuo vikuu kuleta mabadiliko ya kitaifa.
“Kwa sasa tunapoteza asilimia 60 ya rasilimali kupitia ufujaji, ikiwa tutaweka pamoja rasilimali hizi, tutaweza kuwasomesha wanafunzi wetu,” alisema Wetangula.
Wetang’ula pia alitoa wito kwa chuo Kikuu cha Daystar, kubuni mkakati utakaotoa suluhu kwa changamoto za mfumo katika sekta hiyo muhimu.
Kwa upande wake, Prof. Ayiro aliunga mkono matamshii ya Wetangula, akidokeza kuwa serikali inapaswa kuboresha jinsi inavyowasiliana na wananchi wake.
“Ikiwa tunahitaji maendeleo, tunapaswa kubadilisha Mawasiliano na ubunifu wa sera,” alisema Prof. Ayiro.