Klabu ya Inter Miami inayoshiriki ligi kuu nchini marekani MLS,imeandaa dhifa ya kumtuza mshambulizi na nahodha wa Argentina Lionell Messi kwa mataji 45 aliyotwaa .
Hafla hiyo imeandaliwa mapema Jumapili baada ya Miami kusajili ushindi wa mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Chicago Fire, na kuatanua uongozi wao kileleni pa jedwali hadi pointi 5, zaidi ya Cincinnati iliyo ya pili baada ya mechi 25.
Ingawa Messi hakucheza kwani angali kuuguza jeraha aliitwa kati kati ya uwanja baada ya mechi na kaundaliwa sherehe za mataji 45, aliyonyakua ikiwemo kombe la Dunia,Copa America mara mbili ,ligi kuu Uhispania mara 10,saba ya Copa Del Ray,saba ya Supercopa de Espana na manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mataji mengine aliyoshinda Messi ni matatu ya Uefa Super Cup,kombe la Dunia mara tatua,Ligi Kuu ya Ufaransa mara mbili ,kombe la Ufaransa mara moja ,Kombe la Marekani mara moja,kombe la dunia kwa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 na pia chini ya miaka 23 na tuzo nane za kibinafsi za Ballon d’or miongoni mwa mataji mengine.