Ini Edo azomewa mitandaoni kwa kuhudhuria sherehe

Edo alihudhuria sherehe ya kuadhimisha siku za kuzaliwa nchini Ghana, saa chache baada ya kuzika babake mzazi nchini Nigeria.

Marion Bosire
1 Min Read

Mwigizaji wa Nollywood Ini Edo ameangaziwa mitandaoni kwa njia isiyo nzuri kutokana na hatua yake ya kuhudhuria sherehe ya kuadhimisha siku za kuzaliwa nchini Ghana, saa chache baada ya kuzika babake mzazi.

Wafuasi wa mrembo huyo wa Nigeria mitandaoni wametaja machozi yake wakati wa mazishi ya babake kuwa ya bandia kwa sababu aliamua kusafiri hadi Ghana kuhudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa ya mkwasi Richard Nii-Armah Quaye.

Quaye ametimiza umri wa miaka 41,  na sherehe ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa ilijaa watu mbali mbali maarufu huku burudani ikitolewa na wanamuziki kama Davido na Diamond.

Video inayomwonyesha  Ini Edo akiwa kwenye hafla hiyo ilisambazwa mitandaoni ambapo watumizi wa mitandao walitoa maoni mbali mbali wengi wakimkashifu.

Albert Nat Hyde, ndiye alichapisha video hiyo kwenye mtandao wa X ambapo Ini Edo alionekana akiwa amevaa mavazi ya rangi nyeusi na amebeba mkoba wa rangi ya fedha.

Kulingana na Hyde, machozi ya Ini kwenye mazishi ya babake huko Akwa Ibom Machi 21, 2025 hayakuwa ya kweli.

Katika sherehe hiyo Richard Nii-Armah Quaye alipokea magari matatu ya kifahari kati ya zawadi nyingine nyingi.

Website |  + posts
Share This Article