Derby nambari 96 ya mashemeji baina ya AFC Leopards na Gor Mahia hatimaye itasakatwa leo alasiri katika uchanjaa wa kitaifa wa Nyayo.
Itakuwa mara ya kwanza kwa mahasimu hao kukutana msimu huu wakiwania alama tatu za Ligi Kuu ya FKF ,baada ya kuahirishwa mara mbili.
Mkwangurano huo utaanza kutifua vumbi saa kumi huku Gor ,maarufu K’ogalo wakijivunia ubabe wa derby hiyo wakishinda mechi 33,Chui wakiibuka kidedea mara 28 huku mechi 34 zikiishia sare.
Mabingwa watetezi Gor wanashikilia nafasi ya tatu ligini kwa pointi 42,alama sita juu ya watani wao wa leo walio katika nafasi ya tano