Rais wa shirikiso la soka Duniani FIFA,Gianni Infantino, ameipongeza Gor Mahia, kwa kunyakua taji ya Ligi Kuu Kenya msimu wa mwaka 2025/2026.
Gor Mahia walishinda taji ya Ligi Kuu Kenya kwa mara ya 22 wiki iliyopita, baada ya wapinzani wa karibu AFC Leopards kushindwa na APS Bomet FC.
K’ogalo wanaongoza jedwali kwa alamna 69, kuelekea kwa mechi ya kufunga msimu Jumapili ya Mei 31.
Kufuatia ushindi huo Gor wataiwakilisha Kenya katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.
