Serikali imetangaza kesho Ijumaa Oktoba 17 kuwa siku ya mapumziko kwa heshima ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliyefariki mapema Jumatano akiwa nchini India kwa matibabu.
Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen, kupitia kwa gazeti rasmi la serikali, alitangaza Ijumaa kuwa siku kuu kutoa fursa kwa Wakenya kumwomboleza marehemu Odinga.
Mazishi ya kitaifa yameratibiwa kuandaliwa Ijumaa katika uwanja wa Nyayo, kabla ya mwili kupelekwa Bondo kwa mazishi yatakayoandaliwa Jumapili eneo la Bondo.
Baba Aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 80 akiacha pengo kubwa la kisiasa kutokana na mchango wake wa kuleta demokrasia.