Idriss Deby ashinda Urais wa Chad

Dismas Otuke
0 Min Read

Kiongozi wa kijeshi Mahamat Idriss Deby Itno,ametangazwa mshindi wa Urais nchini Chad kulingana na matokeo yaliyotangazwa na shirika linalosimamia kura nchini humo.

Deby aliye na umri wa miaka 40 alipata asimilia 61.03 ya kura zote zilizopigwa akiwashinda wapinzani wengine tisa waliokuwa wakiwania kiti hicho.

Mpinzani wa karibu wa Deby alikuwa Waziri Mkuu Succes Masra,aliyepata asilimia 18.53 ya kura zote ingawa amepinga matokeo ya uchaguzi huo.

Share This Article