Idara ya Uhamiaji imeendeleza zoezi la usajili wa Wakenya kuchukua vitambulisho vya kitaifa maarufu kama Usajili Mashinani.
Maafisa wa idara hiyo walizuru taarafa ya Laisamis kaunti ya Marsabit mwishoni mwa juma na kuwasaidia wasio na vitambulisho kujisajili bila malipo.
Hatua hiyo ya serikali inalenga kuwapunguzia wananchi mzigo wa kusafiri kwa mwendo mrefu hadi vituo vya kujisajili ili kupata kitambulisho cha kitaifa.
Ni wiki ya pili tangu serikali ianzishe zoezi hilo.
Zoezi sawi liliandaliwa katika kaunti za Samburu na Isiolo katika juhudi za kuleta huduma karibu na wananchi.