Idara ya uhamiaji imentangaza kuchapisha shughuli ya utoaji pasipoti kuanzia kesho Mei 13 hadi Ijumaa tarehe 18, katika vituo vyote vya kuchapisha pasipoti nchini.
Idara ya uhamiaji kwenye arifa, ilisema shughuli hiyo itaharakishwa katika vituo vya Nairobi, Mombasa, Kisumu, Eldoret, Embu, Nakuru, Kisii na Kericho.
Takriban pasipoti 720,000 zilikuwa zimecheleweshwa kuchapishwa.
Waziri wa usalama wa kitaifa Prof. Kithure Kindiki, alisema mchakato wa kuchapisha pasipoti mpya, utaharakishwa baada ya serikali kununua mashine mbili mpya.