Takwimu zilizotolewa hivi maajuzi nchini Uganda, kuhusu idadi ya wanachama wa vyama vya kisiasa imezua hofu nchini humo wengi wakihisi kuhadaiwa.
Kulingana na ripoti hiyo, chama tawala cha National Resitance Movement (NRM), National Unity Platform (NUP), Forum for Democratic Change (FDC), na Uganda Peoples Congress (UPC) vina jumla ya wanachama milioni 46.2.
Kinaya ni kuwa Uganda ina idadi ya watu milioni 45.9 kwa mujibu wa sensa ya kitaifa ya watu ya mwaka jana.
Watafiti na wadadisi wengi wamesema takwimu hizo za idadi ni za uongo na zisizo na mashiko kwani idadi ya wanachama wa vyama kamwe haiwezi kuzidi idadi ya watu.
Uganda inatarajiwa kuandaa uchaguzi mkuu Januari 12 mwaka ujao.