Idadi ya waliofariki baada ya kunywa pombe haramu Migori yafika 12

Tom Mathinji
1 Min Read

Idadi ya watu waliofariki baada ya kubugia pombe haramu iliyo na sumu kaunti ya Migori imeongezeka hadi 12.

Jana Jumatano, watu wengine wanne waliangamia walipokuwa wakipokea matibabu katika hospitali ya Samjomen katika eneo la Mabera, Kuria Magharibi.

Kulingana na wakazi, waliofariki walikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakibugia pombe usiku kucha kabla ya kukumbwa na matatizo ya kupumua na kuongea.

Wakazi hao sasa wanatoa wito kwa maafisa wa utawala kutokomeza zimwi la pombe haramu katika eneo hilo.

Website |  + posts
Share This Article