Ibada ya mazishi ya marehemu Hayati Raila Amolo Odinga itafanyika Jumapili katika Chuo Kikuu cha Jaramogi Oginga Odinga.
Ibada hiyo imeratibiwa kuandaliwa kati ya saa tatu asubuhi hadi saa saba adhuhuri.
Baadaye mwili wa marehemu utapelekwa nyumbani kwake kwa mazishi.
Raila alifariki Jumatano wiki hii akiwa na umri wa miaka 80 nchini India alipokuwa ameenda kwa matibabu.