Huduma za mfumo wa e-Citizen zarejea

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imetangaza kurejea kwa huduma zote za mtandaoni kupitia mfumo wa e-Citizen kufuatia jaribio la udukuzi lililositisha baadhi ya huduma.

Huduma zaidi ya 5,000 za serikali zinapatikana kwenye mfumo huo.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Wizara ya Usalama wa Taifa, hamna habari zozote muhimu zilizopotea wala kuhitilafiwa wakati wa jaribio hilo.

Serikali imetoa hakikisho kuwa itatoa huduma kamili,  za kuaminika na salama za mtandaoni.

Pia kampuni ya Kenya Power ilitangaza kudukuliwa kwa mtandao wake wa kulipia umeme.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *