Huduma ya Polisi yafafanua kuhusu ufurushaji wa wakazi eneo la Nyamavila, Kayole

Katika taarifa iliyotiwa saini na Resila Onyango msemaji wa polisi, huduma ya taifa ya polisi inaelezea kwamba ubomozi huo wa majengo unahusiana na mgogoro wa kisheria wa muda mrefu kuhusu ardhi ya kampuni ya Muthithi Investment.

Marion Bosire
2 Min Read

Huduma ya Taifa ya Polisi, NPS imefafanua kuhusu ufurushaji wa wakazi unaoendelea katika eneo la Nyamavila huko Kayole, kaunti ya Nairobi, ulioanza Jumatatu, Desemba 16, 2024.

Katika taarifa iliyotiwa saini na msemaji wa polisi Resila Onyango, huduma hiyo inaelezea kwamba ubomozi huo wa majengo unahusiana na mgogoro wa kisheria wa muda mrefu.

Mgogoro huo ni kuhusu ardhi ya kampuni ya Muthithi Investment, yenye nambari ya usajili LR. No. 23917 Nairobi, kulingana na agizo la mahakama lililotolewa Mei 2013.

Kulingana na Huduma ya Polisi ya Taifa, ufurushaji huo unafuata uamuzi wa kesi ya Mahakama ya Mazingira na Ardhi nambari. 457 ya 2013.

Mahakama ilielekeza kwamba washtakiwa, ambao ni Andrew Kyendo, Amina Mohamed na William Mwangangi, waondoke kwenye ardhi hiyo kwa kushindwa kutii masharti ya kisheria yaliyowekwa awali.

Agizo hilo lilielekeza kuondolewa kwa watu na miundombinu kutoka kwenye eneo hilo.

Tamko hilo lilithibitisha kwamba eneo hilo, ambalo awali lilikuwa na vipande 304 vya ardhi, lilikuwa limetolewa notisi za kuhamishwa.

Wamiliki wengi wa vipande hivyo walitii agizo hilo kwa kulipa na kupokea hati za umiliki wa ardhi, lakini wachache walibaki kinyume na sheria.

Kufuatia taratibu za kisheria, uvamizi ulifanywa kati ya Desemba 16 na 18, 2024.

Huduma ya Polisi ya Taifa inasisitiza kujitolea kwake katika utekelezaji wa sheria kwa ufanisi, ikisema kwamba operesheni hii ilifanyika kwa uwazi na kwa njia halali.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *