Hospitali ya rufaa ya Kilifi yapokea vifaa vya matibabu ya meno kutoka Marekani

Marion Bosire
1 Min Read

Hospitali ya rufaa ya kaunti ya Kilifi imenufaika na vifaa vya kisasa vya matibabu ya meno kutoka Marekani.

Naibu balozi wa Marekani nchini Kenya Mark Dillard, ndiye aliwasilisha vifaa hivyo kutoka kwa jeshi la Marekani hususan wanajeshi wanaohudumu katika ubalozi wa Marekani nchini Kenya.

Akizungumza wakati wa kupokea vifaa hivyo, Gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro alishukuru Marekani kwa juhudu zinazoendelea za kuimarisha huduma za Afya nchini.

Kulingana na Mung’aro shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani USAID linatekeleza jukumu muhimu katika kusaidia kuboresha huduma hizo.

Gavana Mung’aro amefafanua pia kwamba walijadiliana na ujumbe huo wa Marekani ambapo waligusia fursa zilizopo za uwekezaji katika kaunti ya Kilifi.

Walizungumzia pia nyanja ambazo wanaweza kushirikiana ili kuchangia katika ajenda ya maendeleo kwa lengo la kuboresha maisha ya wakazi.

Mung’aro kama kiongozi wa serikali ya kaunt ya Kilifi, aliahidi kuhakikisha kwamba wakazi wote wa Kilifi wanapata huduma bora na za kisasa za matibabu ya meno katika hositali zote za kaunti.

Share This Article