Hospitali ya rufaa na utafiti ya Chuo Kikuu cha Kenyatta (KUTRRH),imedhinishwa kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosomea kozi ya dawa katika chuo kikuu cha Kenyatta.
Chuo hicho kimepokea idhini kutoka kwa Baraza la wahudumu wa afya na dawa nchini (KMPDC).
Leseni hiyo itadumu kwa kipindi cha miaka mitatu ikiwa hatua kubwa ya chuo kikuu cha Kenyatta na wanafunzi wanaosomea kozi ya utabibu .
Chuo kikuu cha Kenyatta kinajiunga na vyuo vingine vilivyoidhinishwa kwa mafunzo hayo ikiwemo Chuo Kikuu cha teknolojia ya Kilimo cha Jomo Kenyatta( JKUAT),chuo Kikuu cha Nairobi,USIU-A,Chuo kikuu cha AMREF ,chuo kikuu cha Egerton ,chuo kikuu cha Moi ,chuo kikuu cha Mount Kenya,chuo kikuu cha jeshi ,chuo cha Nairobi Women’s , na chuo kikuu cha Mama Ngina .