Hezbollah yathibitisha kifo cha kamanda Ali Karaki

Tom Mathinji
1 Min Read

Hezbollah imethibitisha kifo cha Ali Karaki, kamanda wa kikosi kinachopigana katika eneo la kusini mwa taifa hilo.

Hatua hii inatokea baada ya kauli ya jeshi la Israel (IDF) hapo jana kwamba kamanda huyo alikuwa ameuawa katika shambulizi ambalo lilimuua Nasrallah.

Kundi hilo linaloungwa mkono na Iran, sasa limethibitisha kifo cha Karaki kupitia mtandao wa Telegram.

Israel nayo imesema iliwaua viongozi wengine 20 wa Hezbollah wa nyadhifa tofauti walipomuua Hassan Nasrallah katika makao makuu ya kundi hilo siku ya Ijumaa.

Kama tulivyoripoti, majina hayo ni pamoja na Ali Karaki, kiongozi wa eneo lake la kusini.

IDF pia inasema ilimuua Ibrahim Hussein Jazini, mkuu wa kitengo cha usalama cha Nasrallah, na Samir Tawfiq Dib, ambaye IDF inamtaja kama “msiri na mshauri wa muda mrefu wa Nasrallah”.

Jeshi linaongeza kuwa makao makuu ya Hezbollah yaliwekwa chini ya majengo kadhaa ya raia.

Share This Article