NRF kuandaa kikao cha kila mwaka cha mabaraza ya kutoa ruzuku za kisayansi Afrika

Dismas Otuke
1 Min Read

Hazina ya kitaifa ya utafiti – NRF itaandaa kikao cha kila mwaka cha mabaraza ya kutoa ruzuku za Kisayansi barani Afrika, SGCI kuanzia Jumatatu Novemba 13 hadi Ijumaa Novemba 17.

Kikao hicho kitatoa fursa kwa washirika kujadiliana kwa mapana kuhusu sayansı, teknoljia na uvumbuzi na kutangamana na washirika wengine kama vile wasomi, wadau wa viwanda, mashirika ya kijamii, serikali na mashirika ya kiserikali.

“Kupitia kikao hiki, SGCI na NRF wanapanga kuandaa mafunzo ya moja kwa moja na kufafanua kuhusu mikakati ya utafiti na maendeleo kwa lengo la kuimarisha mabaraza ya sayansi na wadau na jinsi ya kusimamia ruzuku za utafiti,”amesema Prof. Dickson Andala, Afisa Mkuu Mtendaji wa NRF.

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu anatarajiwa kutoa hotuba kuu kwenye kikao hicho.

Share This Article