Mahakama ya Rufaa inatarajiwa kutoa uamuzi leo Ijumaa kuhusu kesi iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha Profesa Njuguna Ndung’u kupitia kwa Mwanasheria Mkuu Justin Muturi ikitaka kuondolewa kwa agizo lililowekwa la kuzuia utekelezaji wa sheria ya fedha ya mwaka 2023.
Sheria hiyo inapendekeza kuongezwa kwa ushuru wa thamani kwa mafuta kutoka asilimia 8 hadi 16, ushuru wa nyumba wa asilmia 1.5 kwa wafanyakazi wote, ushuru kwa wasanii na watumiaji wa mitandao ya burudani miongoni mwa matozo mengine.
Kesi ya kupinga utekelezaji wa sheria hiyo iliwasilishwa mahakamani na Seneta wa Busia Okiya Omtatah.
Wengi wameteta kuwa matozo hayo mapya yatadumaza mifuko yao huku gharama ya bidhaa ikitarajiwa kupanda.