Harry Kane hauzwi ng’o, yasema Tottenham

Dismas Otuke
1 Min Read

Harry Kane amearifiwa na klabu ya Tottenham Hotspur kuwa hatauzwa msimu huu licha ya klabu ya Bayern Munich kuonyesha nia ya kumsajili.

Munich inadaiwa kutoa ada ya dola milioni 76 nukta 6 ili kupata sahihi ya mwanandinga huyo aliye na umri wa miaka 29.

Manchester United pia wanapiga dira kuona kama nahodha huyo wa Uingereza atapigwa bei ili kuwania saini yake msimu wa sasa wa uhamisho wa wachezaji.

Website |  + posts
Share This Article