Timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars imewasili Abidjan,nchini Ivory Coast kwa mchuano wa mwisho wa kundi F kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya wenyeji Jumanne ijayo.
Kikosi cha Harambee Stars kiliondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mapema Jumamosi.
Ivory Coast wanahitaji ushindi ili kufuzu kwa Kombe la Dunia na kuwafungia nje wapinzani wao wa karibu Gabon.
Kenya ni ya nne kundini humo kwa alama 11.
Harambee Stars iliwashinda Burundi bao moja kwa bila katika mchuano wa Alhamisi wiki hii mjini Bujumbura.