Timu ya ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars imeanza vyema makala ya nane ya fainali za CHAN kwa ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya DR Congo katika mechi ya kundi A uwanjani Kasarani Jumapili.
Austin Odhiambo aliwaweka vijana wa Benni McCarthy, kifua mbele kwa goli la dakika ya mwisho ya ziada kipindi cha kwanza kupitia kwa Austin Odhiambo.
Licha ya mabadiliko na mashambulizi ya Congo katika kipindi cha pili kipa wa Kenya Byrne Omondi alikaa ngumu na kuhakikisha harambee Stars ushindi.
Kenya sasa wanaangazia mechi ya pili dhidi ya Angola Alhamisi usiku .