Harambee Stars yaiadhibu Ushelisheli mabao 5-0

Tom Mathinji
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka Harambee stars iliishinda Ushelisheli mabao  5-0 kwenye mechi ya kundi F ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026 iliyochezwa katika uwanja wa Felix Houphouet-Boigny Abidjan, Ivory Coast.

Kenya ilikuwa na matumaini makubwa ambapo nahodha Michael Olunga alifunga mabao mawili ya kwanza katika dakika za kwanza 10.

Masoud Juma alifunga la bao la tatu baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Johana Omollo.

Katika kipindi cha pili, mlinzi Aboud Omar alimwandalia pasi Rooney Otieno na kufunga bao la nne kabla ya mshambulizi wa Gor Mahia Benson Omalla kufunga la tano.

Kenya sasa inashikilia nafasi ya tatu kwa alama tatu katika kundi hilo.

Share This Article