Harambee Stars yaendeleza mazoezi tayari kwa mechi ya Sudan Kusini

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya ,Harambee Stars imeendeleza maozezi yake Ijumaa jioni katika uwanja wa Nelson Mandela jijini Kampala Uganda.

Stars inayoongozwa na kocha Engin Firat itashuka uwanjani Nelson Mandela Jumapili jioni dhoidi ya Sudan kwa mechi ya marudio raundi ya kwanza kufuzu kwa fainali za kombe la Afrika kwa wachezaji wanaoshiriki ligi ya nyumbani.

Kenya ilipoteza mabao 2-0 katika duru ya kwanza  iliyosakatwa wiki jana mjini Juba.

Website |  + posts
Share This Article