Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imeendeleza mazoezi kujiandaa kwa mashindano ya kuwania Kombe la Mapinduzi kisiwani Zanzibar kuanzia mwishoni mwa juma hili.
Stars ambayo iliripoti kambini Jumamosi iliyopita imeanza mazoezi kwa siku ya tatu leo katika uwanaj wa Mpesa Foundation Academy.
Kikosi cha kocha Francis Kimanzi kilicho na wachezaji 37 kitachujwa kabla ya kusafiri kwa mashindano ya Kombe la Mapinduzi kati ya tarehe 3 na 13 mwezi ujao.
Kenya itafungua mashindano hayo dhidi ya Burundi Jumapili hii, Januari 5, kabla ya kukabliana na wenyeji Zanzibar Jumanne.
Kimanzi anatumia pia mashindano ya Mapinduzi kuandaa timu ya Kenya itakayoshiriki fainali za kombe la CHAN mwezi Februari mwakani.