Timu ya taifa ya soka ya Kenya-Harambee Stars itawaalika Sudan Kusini katika mechi ya kimataifa ya kirafiki Jumanne alasiri katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.
Mchuano huo utakuwa wapili wa kujipima nguvu kwa Kenya baada ya kuwashinda wenyeji Qatar mabao 2-1 Ijumaa iliyopita .
Harambee Stars wanatumia mechi hizop za kirafiki kujinoa makali kwa mechi za makundi za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka 2026.
Kenya imejumuishwa kundi moja na majirani Burundi ,Ushelisheli,Ivory Coast na Gabon.
Timu ya taifa imeratibiwa kufungua ratiba dhidi ya Gabon ugenini mwezi Novemba mwaka huu kabla ya kuzuru ushelisheli mwezi huo katika pambano la pili.
Mechi za kufuzu zitakamilika Oktoba mwaka 2025 huku timu bora katika kila kundi ikijikatia tiketi kwa fainali za kombe la dunia za mwaka 2026 zitakazoandaliwa kwa pamoja na mataifa ya Canada,Mexico na Marekani.