Harambee Stars kukabana koo na Burkinabe leo Mapinduzi Cup

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, itashuka uwanjani Gombani kisiwani Pemba, leo usiku kumenyana na Burkinafaso kuwania kombe la Mapinduzi.

Stars inayofunzwa na kaimu kocha Francis Kimanzi inatumia mashindano hayo kujiandaa kwa kipute cha CHAN mwezi ujao.

Kenya iliwasili Zanzibar juzi kwa mashindano hayo ya mataifa manne.

Harambee Stars watarejea uwanjani Jumanne kwa mechi ya pili dhidi ya Tanzania bara ,kabla ya kuhitimisha ratiba Ijumaa ijayo dhidi ya wenyeji Zanzibar.

Wakati uo huo Zanzibar walifungu kipute hicho kwa ushindi wa bao moja kwa bila jana dhidi ya Tanzania bara.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *