Harambee Stars kuingia kambi Oktoba 4 kwa mtihani wa Cameroon

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya Kenya-Haram ee Stars itaripoti kwa kambi ya mazoezi Ijumaa Oktoba 4, kujiandaa kwa mechi za kufuzu AFCON dhidi ya Cameroon.

Kikikosi hicho cha kocha Engin Firat kinawajumuisha wachezaji 288 ambao watachujwa hadi 23 wa mwisho.

Stars imepigwa jeki na kurejea kwa nahodha Michael Olunga ambaye alikosa mechi ya mwezi jana dhidi ya Namibia kutokana na jeraha.

Kenya itachuana na Indomitable Lions ya Cameroon Oktoba 11 katika uwanja wa Japoma mjini Doula, kabla ya kuwaalika Cameroon kwa pambano la marudio siku tatu baadaye katika uchanjaa wa Nelson Mandela mjini Kampala Uganda.

Cameroon na Kenya wanaongoza kundi J kwa alama 4 kila moja baada ya mechi mbili.

Timu mbili bora kutoka kundi hilo zitafuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika AFCON mwaka ujao nchini Morocco.

Share This Article