Harambee Starlets yapigwa kitutu nchini Morocco

Kenya walitumia mchuano huo kama matayarisho ya mwisho kwa michuano ya CECAFA

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka ya Kenya kwa wanawake Harambee Starlets, iliambulia kichapo cha mabao 5-1, na wenyeji Morocco katika mchuano wa kimataifa wa kirafiki uliosakatwa jana usiku mjini Tangier.

Kenya walitumia mchuano huo kama matayarisho ya mwisho kwa michuano ya CECAFA, itakayoandaliwa jijini Dares Salaam, Tanzania, kuanzia wiki ijayo.

Upande wao Atlas Lionesses, walitumia pambano hilo kujiandaa kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika WAFCON mwezi ujao.

Website |  + posts
Share This Article