Timu ya taifa ya soka Harambee Stars, imeendeleza mazoezi kujiandaa kwa mechi ya pili ya kuwania kombe la Mapinduzi kesho dhidi ya Tanzania bara.
Stars chini ya uongozi wa kaimu kocha Francis Kimanzi, ilitoka sare ya bao 1 dhidi ya Burkinafaso, katika mchuano wa ufunguzi Jumamosi iliyopita.
Kenya itahitimisha ratiba kwa kukabiliana na wenyeji Zanzibar Heroes Ijumaa hii.
Kenya na Tanzania wanatumia mashindano hayo kujiandaa kwa michuano ya CHAN, itakayoandaliwa kati ya tarehe 1 na 28 mwezi ujao.
Mechi ya kesho itakuwa ngumu hususan ,baada ya Tanzania kushindwa bao 1 kwa bila na wenyeji Zanzibar Ijumaa iliyopita.