Kundi haramu la Kipalestina ,Hamas limewaachilia huru mateka 24 wa kwanza likibadilishana na wafungwa wa Palestina walio katika magereza ya Israel.
Haya yalijiri baada ya mwafaka wa kusitisha mapigano kati ya Hamas na wanajeshi wa Israel kuafikiwa wiki hii.
Mateka hao ni pamoja na Waisraeli 13, Wathailand 10 na Wafilipino wawili.
Kundi la Hamas lilitoa ukanda wa video ulioonyesha wanaume wakiwa wamejihami kwa bunduki na kufunika nyuso zao wakiwaachilia huru mateka.
Israel pia ilitimiza makubaliano hayo kwa kuwaachilia huru wafungwa wa Palestina 39, wakiwemo wanawake na watoto kutoka kwa magereza yake.
Mateka walioachiliwa huru na Hamas walikabidhiwa kwa maafisa wa shirika la msalaba mwekundu waliowapeleka hospitalini kupokea matibabu.
Vita vya Israel Hamas vimedumu kwa majuma saba na kusababisha vifo vya Waisraeli wapatao 3,000 na Wapalestina 15,000 ,na vilisitishwa juma hili kufuatia mazungumzo kati ya Misri,makundi haramu ya Palestina,Marekani,Israel na Qatar.