Hakimu apigwa risasi wakati wa kikao cha mahakama Makadara

Marion Bosire
1 Min Read
Mahakama ya Makadara.

Hakimu mmoja alipigwa risasi na kujeruhiwa siku ya Alhamisi katika Mahakama ya Makadara jijini Nairobi.
Kulingana na polisi, Hakimu huyo wa mahakama ya Makadara Monica Kivuti, alipigwa risasi na afisa wa polisi wakati wa kikao cha mahakama ambapo alikuwa akitoa uamuzi katika kesi iliyomhusisha mke wa afisa huyo.

Maafisa wengine wa polisi waliokuwepo wakati wa kisa hicho, walijibu kwa kumpiga risasi afisa huyo aliyetambulika kama Inspekta Samson Kipruto, na kumuua papo hapo.

Kipruto anaripotiwa kukasirishwa na uamuzi wa hakimu wa kutupilia mbali dhamana aliyopewa mkewe. Mkewe afisa huyo, Jenniffer Wairimu mwenye umri wa miaka 48, alishtakiwa katika kesi ya kupata shilingi milioni 2.9 kwa njia ya ulaghai. Alikuwa ameomba kuachiliwa kwa dhamana ya pesa taslimu, lakini mahakama haikukubali.

Kulingana na ripoti ya polisi, Inspekta Kipruto aliingia ndani ya mahakama kupitia mlango wa hakimu na kufyatua risasi kuelekea kwa hakimu na kumjeruhi kifuani na kiuno cha kushoto.

Maafisa wa upelelezi wametembelea eneo la tukio hilo na kuanzisha uchunguzi.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *