Hafla ya mazishi yageuka kuwa jukwa la vurumai

Tom Mathinji
1 Min Read

Hafla ya mazishi ya aliyekua mtangazaji wa kituo kimoja cha redio eneo la Pwani Sammy Ambari, iligeuka kuwa uwanja wa vita baada ya mwakilishi wadi ya matsangoni Hassan Mohamed, kukabiliana vikali na mwakilishi wa wanawake kaunti ya kilifi Getrude mbeyu.

Fujo zilianza wakati mwakilishi huyo wa wadi ya matsangoni Hassan Mohamed alipompokonya kinasa sauti Mbeyu alipokua akitoa rambi rambi zake kwa mamia ya waombolezaji ambao walikua wamejitokeza kwa mazishi hayo.

Katika vuta ni kuvute hiyo baina ya mbeyu na Hassan ambao nusra wapigane hadharani, walinzi wa Mbeyu na wafuasi wake walijitokeza na kuwatenganisha viongozi hao wawili.

Waziri wa usawa na jinsia Aisha Jumwa ambaye pia alihudhurua mazishi hayo, aliingilia kati kutuliza hali, huku akiwamuru polisi kutuliza vurugu ambazo zilizuka.

Gavana wa kaunti ya kilifi Gideon Mng’aro alisalia kimya kwenye sintofahamu hiyo japo aliwataka viongozi kuwa makini kwenye semi zao hasa katika hafla za mazishi.

Share This Article